ATCL kuanza safari kutoka Dar es salaam kwenda Chato

0
243

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Januari 9 mwaka 2021 itaanza rasmi safari za ndege kutoka Dar es salaam kwenda Chato mkoani Geita na kutoka Chato kwenda Dar es salaam.

Mkurugemzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi amewaambia Waandishi wa habari mkoani Geita kuwa, kwa kuanzia wataanza safari mara mbili kwa wiki siku za Alhamisi na Jumamosi.

Amesema kuwa, kuanzia Januari 18 mwaka 2021 safari hizo zitaongezwa na kuwa mara tatu kwa wiki katika siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.