Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba wamemsimamisha kiungo wake wa kati Jonas Mkude
kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili
Taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika Barbara Gonzalez inaeleza kuwa Simba imefikia kuchukua maamuzi hayo kwasababu haina uvumilivu na
utovu wa nidhamu kwa sababu ndio uti wa mgongo wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini
Taarifa hiyo haijaeleza bayana ni vitendo gani vya utovu wa nidhamu ambavyo Jonas Mkude anatuhumiwa kuvifanya lakini inasema kusimamishwa kwake kunapisha uchunguzi zaid juu ya tuhuma hizo.