Watalii zaidi kuitembelea Tanzania

0
267

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro amesema Tanzania tayari imeweka mikakati imara na madhubuti kupokea watalii zaidi ya milioni 5 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025.

Dkt Ndumbaro ameyasema hayo katika uwanja wa ndege jijini Arusha, alipowakea Watalii waliokuja nchini kwa ajili kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii.

Watalii hao kutoka nchini Marekani watatembelea hifadhi za Serengeti na Ngorongoro, akiwemo muandaaji maarufu wa taarifa na makala za Utalii duniani, -Drew Binsky.