Waumini wa dini ya Kikristo nchini, leo wanaungana na wenzao wa Mataifa mbalimbali duniani kusherehekea sikukuu ya Krismasi.
Sikukuu ya Krismasi inasherehekewa ikiwa ni kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Misa ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi Kitaifa ilifanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Watakatifu Wote jimbo Katoliki la Mtwara.
Kitaifa Misa ya Krismasi inafanyika mkoani Mtwara katika Kanisa la Biblia Tanzania na kuongozwa na Askofu John Mchopa.
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kupitia vyombo vyake vya Redio na Televisheni, linarusha moja kwa moja matangazo hayo ya Misa ya Krismasi kutoka mkoani Mtwara.