Waziri Mkuu wa Ethiopia, – Abiy Ahmed amepeleka vikosi vya jeshi katika jimbo la Benishangul-Gumz lililopo Magharibi mwa nchi hiyo.
Abiy amefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya watu wenye silaha kuwaua zaidi ya watu mia moja katika jimbo hilo ambalo limekuwa likikumbwa na mapigano ya mara kwa mara ya kikabila.
Habari zaidi kutoka nchini Ethiopia zinaeleza kuwa, tayari jeshi la nchi hiyo limewaua watu 42 wenye silaha, wanaodaiwa kuhusika na mauaji hayo.
Tume ya Haki za Binadamu ya Ethiopia imeeleza kuwa mauaji hayo yametokea katika kijiji cha Bekoji.
Watu walioshuhudia mauaji hayo wamesema kuwa nyumba kadhaa zimechomwa moto, huku watu wengi wakichomwa miili yao na silaha zenye ncha kali.