Msitumie pesa nyingi wakati wa sikukuu – RC Byakanwa

0
163

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, amewaasa Watanzania kutotumia pesa nyingi kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kwani mapema mwezi Januari 2021 shule zinafunguliwa na watoto watahitaji mahitaji ya shule.

Byakanwa amezungumza hayo wakati akifanya mahojiano na TBC kuelekea sherehe za sikukuu ya Krismasi zinazofanyika kitaifa mkoani humo.

“Niwasihi Watanzania kutotumia pesa nyingi kipindi hiki cha sikukuu kwani ni wiki moja tu baada ya hapo wanafunzi watahitaji kurudi shule kwa hiyo tuwe na tahadhari,” amesema Byakanwa.

Kuhusu hali ya usalama msimu huu wa sikukuu, Byakanwa amesema usalama umeimarishwa ndani ya mkoa wa Mtwara, hivyo watu mbalimbali wanakaribishwa kutembelea mkoa huo.

“Hali ya ulinzi na usalama ni ya kuridhisha, wageni wote tunawakaribisha mfike mkoani kwetu kwa ajili ya matembezi kwani yapo maeneo mengi ya kutembelea”,Amesema Byakanwa.

Sherehe za Krismasi kwa mwaka 2020 zinafanyika kitaifa mkoani Mtwara huku Amani na Upendo ukisisitizwa.