DAWASA yafanya mabadiliko ya Watendaji

0
434

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja, amefanya mabadiliko ya Watendaji katika nafasi mbalimbali ndani ya Mamlaka hiyo pamoja na kuongeza mikoa Saba, lengo likiwa ni kuboresha utoaji huduma.

Mhandisi Luhemeja ametangaza mabadiliko hayo leo, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la  Waziri wa Maji  Jumaa Aweso alilolitoa jana  la kumtaka kufanya mabadiliko  hayo ikiwa ni pamoja na nafasi za Mameneja ili kuboresha huduma za upatikanaji wa maji.

Waziri Aweso alitoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea mradi wa tanki la maji Pugu pamoja na uzinduzi wa huduma ya maji kwa Wakazi wa Kifuru.

Alitaka kufanyika mabadiliko kwa Watendaji wa DAWASA wa Tabata, Temeke, Tegeta, Ilala, Magomeni, Kigamboni, Mkuranga,  Kisarawe, Mbezi, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Ubungo, Kinondoni na Ukonga.

Kwa mujibu wa Waziri Aweso, wapo baadhi ya Watendaji wa DAWASA si waaminifu na wamekuwa wakitumia vibaya fedha za miradi ya maji na kusababisha maeneo mengi kukosa huduma ya maji.