Simba yapoteza ugenini

0
192

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Simba, wamepoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya FC Platnum ya Zimbabwe kwa kufungwa bao 1 kwa bila.

Bao pekee katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Taifa nchini Zimbabwe, limefungwa na kiungo Perfect Chikwende dakika ya 17 ya mchezo huo.

Simba sasa inajipanga kwa ajili ya mchezo wa marejeano utakaopigwa nchini Tanzania.