Serikali ina mpango wa kuaandaa mfumo shirikishi na endelevu wa kudhibiti uvuvi haramu, ambao utaifanya mikoa na wilaya zishiriki kikamilifu katika kutokomeza uvuvi huo, badala ya kuwa na operesheni za kutafuta wavuvi haramu.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, – Mashimba Ndaki wakati wa mkutano wake wa hadhara na wakazi wa kijiji cha Mchinga Namba Mbili kilichopo mkoani Lindi.
Amesema mfumo huo utaisaidia serikali kuondokana na operesheni za vipindi maalumu na kuwa na mfumo unaofanya kazi siku zote.
Waziri Ndaki amewataka watu wanaojihusisha na wanaofikiria kujiingiza katika uvuvi haramu watatafutwe popote walipo na wachukulie hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
Pia amewapongeza wananchi wanaoishi Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi kwa kudhibiti uvuvi haramu hasa unaotumia mabomu.
Kuhusu zao la mwani Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi amezitaka kampuni zinazonunua zao hilo kutumia mizani sahihi na kuacha mara moja kuwadhulumu wakulima hao wa kijiji cha Mchinga Namba Mbilina, pia amewataka Wakulima kuangalia uwezekano wa kuliongezea thamani zao hilo ili liuzwe kwa bei nzuri.