Kiba kuachia albamu 2021

0
237

Nyota wa muziki nchini, Ali Kiba ameweka wazi kuwa ataachia albumu yake mpya mwaka 2021.

Kiba ameeleza hayo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, ambapo amesema mara ya mwisho kutoa albumu ilikuwa ni mwaka 2008.

“Mara ya mwisho kutoa album ilikuwa 2008, mwakani 2021, nitatoa tena albumu haitofika mwezi wa sita,” amesema Alikiba ambaye ni boss wa lebo ya Kings Music.

Kwa kauli hiyo ya Kiba, anaungana na msanii Lady JayDee ambao wote washatoa ahadi kwa mashabiki wao ya kuachia albumu mwaka 2021.