Arteta akiri hali ngumu Arsenal

0
305

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema hana mpango wa kuikimbia kazi,  na anaamini bado anaungwa mkono na wakuu wa klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Kocha huyo Mhispania amesema anachofikiria kwa sasa ni  kupambana ili kuirejesha timu hiyo kwenye hali nzuri ya kushinda michezo mbalimbali,  hasa ya Ligi Kuu na sio kuondoka.

Arsenal imeshindwa kupata ushindi ndani ya michezo saba, ambapo imepoteza michezo mitano na kutoka sare michezo miwili na imeshuka hadi kwenye  nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi Kuu ya England.

Kwa kinywa chake Arteta anakiri kuwa kwa sasa wanapitia wakati mgumu, ila hakuna namna inabidi wapambane tu ili kuirejeshea heshima timu yao ya Arsenal.

Leo Jumanne Arsenal itacheza na Manchester City kwenye mchezo wa Carabao Cup hatua ya robo fainali, na Arteta anakiri kuwa wanakwenda kwenye mchezo huo huku hali yao ikiwa bado sio nzuri.