Waziri Bashungwa asisitiza ubunifu katika sanaa

0
317

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa ameuagiza uongozi wa chuo cha Sanaa Bagamoyo kuwa wabunifu  kujenga vijana wajiajiri katika sanaa pamoja na kuandaa program mbalimbali zitakazowezesha chuo hicho kujitangaza pamoja na kukiingizia mapato.
 
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati alipotembelea chuo hicho kukagua kazi zinazofanywa na chuo hicho pamoja na hali ya miundombinu  iliyoko chuoni hapo.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha TASUBA Dokta Hebert Makoye amesema chuo hicho kinampango wa kuboresha na kuongeza  kozi nyingi  ili kuwezesha vijana wengi kujiunga na chuo hicho.