Waziri Jafo atilia shaka ujenzi kituo cha mabasi Igumbilo

0
172

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amekagua ujenzi wa jengo la abiria la kituo kikuu cha mabasi cha Igumbilo mkoani Iringa na kubaini fedha nyingi zimetumika kwenye ujenzi wa msingi wa jengo hilo.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemtaka Mhandisi wa Manispaa ya Iringa kumshauri vema Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuepuka kutumia fedha zaidi kwenye miradi ya ujenzi.

Zaidi ya shilingi Bilioni moja nukta mbili zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa jengo hilo la abiria la kituo kikuu cha mabasi cha Igumbilo.