Rashford apiga 2, United ikiitandika Sheffield

0
142

Manchester imesogea hadi nafasi ya 6 katika msimamo ligi kuu England baada ya kuitandika Sheffield United mabao 3 kwa 2

Sheffield walikuwa wa kwanza kuchungulia nyavu za United kupitia kwa David McGoldrick dakika ya 5 na kufunga bao la pili dakika ya 87

Matokeo hayo yalibadilishwa kwa magoli mawili ya Marcus Rashford pamoja na goli moja la Anthony Martial na mchezo kumalizika kwa United kuondoka na alama 3 muhimu wakiwa ugenini katika dimba la Bramall Lane

Kwa matokeo hayo Sheffield wanaendelea kuburuza mkia wakiwa na alama moja huku United wakisogea hadi nafasi ya 6 wakiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 12