Kituo cha mabasi Mwenge kuanza kutumika Machi 2021

0
224

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, -Aboubakar Kunenge ameiagiza Manispaa ya Kinondoni pamoja na mkandarasi kutoka JKT, kuhakikisha ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mwenge na maduka 126 unakamilika kabla ya Februari 28 mwaka 2021 na kuanza kutumika Machi Mosi mwaka 2021.

Kunenge ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali wilayani Kinondoni, ambapo ameielekeza Manispaa ya wilaya hiyo kuhakikisha inampatia mkandarasi fedha kwa wakati ili asipate kikwazo cha kumfanya ashindwe kutekeleza ujenzi huo.

Pia amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es salaam, kuhakikisha ifikapo Februari Mosi mwaka 2021, masoko yote yaliyokamilika yanaanza kutoa huduma, kwa kuwa lengo la ujenzi wake lilikuwa ni kutumika na sio kubaki Kama magofu.