Wazee wa darajani Chelsea (the blues) wameshindwa kutamba mbele ya wenyeji Wolverhampton Wanderers katika dimba la Molineux baada ya kuchezea kichapo cha mabao 2 kwa 1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Mabao ya Wolves yamefungwa na Daniel Podence na Pedro Neto huku bao pekee la Chelsea likifungwa na mshambuliaji Olivier Giroud.
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu England, Manchester City wamelazimishwa sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya West Bromwich Albion katika uwanja wa Etihad.