Rais Dkt John Magufuli leo anaongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri, tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani katika kipindi chake cha pili.
Kikao hicho kinafanyika Ikulu Chamwino mkoani.Dodoma.
Kikao hicho kinahudhuriwa pia na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Katika kikao hicho cha kwanza cha Baraza la Mawaziri pia wamealikwa baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali.