Sudan yaondolewa kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi

0
299

Marekani imeiondoa rasmi Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Taarifa ya Sudan kuondolewa kwenye orodha hiyo imetangazwa na ubalozi wa Marekani nchini Sudan.

Mwezi Oktoba mwaka huu Rais Donald Trump wa Marekani alisema kuwa, Sudan itaondolewa kwenye orodha hiyo ya nchi zinazofadhi ugaidi endapo itakubali kulipa fidia ya Dola Milioni 335 za Kimarekani kwa waathirika wa mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa mwaka 1998 na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda kwenye Balozi za Marekani katika nchi za Tanzania na Kenya.

Waziri Mkuu wa Sudan, – Abdalla Hamdok amethibitisha kulipwa kwa fidia hiyo.

Mwaka 1993, Marekani iliziweka nchi za Sudan, Iran, Korea Kaskazini na Syria  kwenye orodha ya nchi zinazofadhili vitendo vya Kigaidi.