Zanzibar kuendelea kuboresha vivutio vya uwekezaji

0
280

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi, amewahakikishia wawekezaji wanaotaka kuwekeza Zanzibar kuwa Serikali itawawekea mazingira mazuri.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu jijini Zanzibar alipofanya mazungumzo na mmiliki wa hoteli ya Park Hyatt, -Ali Saeed Juma Albwardy kutoka Dubai aliyefuatana na Nicolas Cedro ambaye ni Meneja Mkuu wa hoteli hiyo.

Amesema Serikali anayoiongoza itahakikisha inashirikiana na wawekezaji pamoja na kuwawekea mazingira bora ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa Rais Mwinyi, kwa upande wa sekta ya Utalii ambayo ndio inayochangia zaidi katika pato la Taifa, Serikali yake itahakikisha inawawekea mazingira mazuri wawekezaji wake.

Amesema Serikali ya Zanzibar imekusudia kuendelea kushirikiana na sekta binafsi, kwani inatambua umuhimu wa sekta hiyo katika kukuza uchumi na kuinua pato la Taifa.