Profesa Manya aapishwa kuwa Mbunge

0
218

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amemuapisha Profesa Shukrani Manya kuwa Mbunge wa Bunge hilo.

Profesa Manya ameteuliwa mapema hii leo na Rais John Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania