Uteuzi wa Naibu Waziri wa Madini watenguliwa

0
562

Rais John Magufuli amesema atateua Naibu Waziri mwingine wa Madini baada ya aliyemteua Disemba 5 mwaka huu Francis Ndulane kushindwa kuapa kwa ufasaha.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri ambapo Ndulane alikuwa ni miongoni mwa Naibu Mawaziri waliotakiwa kula kiapo hicho.