Wafungwa 256 waliohukumiwa adhabu ya kifo sasa kufungwa maisha

0
234

Katika kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika, Rais John Magufuli amewapunguzia adhabu Wafungwa 256 waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ambapo kwa sasa watatumikia kifungo cha maisha.

Rais Magufuli pia ametangaza kuwapunguzia adhabu na kuwaachia huru Wafungwa wengine 3, 316 ambao kati yao ni wale wenye makosa madogo na wengine ambao wametumikia kifungo chao kwa muda mrefu na zimebakia siku chache wamalize kutumikia vifungo vyao.

Amewapongeza Watanzania wote kwa kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo Ikulu Chamwino jijini Dodoma baada ya kuwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri aliowateua hivi karibuni.