Jamii imetakiwa kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili na kujenga kizazi chenye uelewa wa masuala ya ukatili.
Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema kuwa, katika maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, wamealika makundi mbalimbali kwa lengo kujadili masuala ya kijinsia pamoja na haki.
Maadhimisho hayo yameshirikisha Wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakijishughulisha na kupinga vitendo vya ukatili.