Nana Akufo Addo aongoza kwa kura za Urais

0
314

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Ghana, kufuatia uchaguzi wa Rais na Wabunge uliofanyika Jumatatu Disemba 7.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa Rais Nana Akufo Addo anayewania kiti cha Urais kwa kipindi cha pili, anaongoza kwa kura katika kinyang’anyiro cha Urais akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu John Mahama ambaye ni Rais wa zamani wa Ghana.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali, chama tawala cha NPP kinaongoza kwa kupata viti vingi vya Ubunge kufuatia uchaguzi huo.