Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania -TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema Chaneli ya Utalii ya Tanzania Safari inaendelea kuboresha vipindi vyake ili viweze kufikia viwango cha kimataifa.
Dkt. Rioba ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa mafunzo yaliyowashirikisha baadhi ya Watendaji wa TBC, ambayo pamoja na mambo mengine yamejikita katika uandaaji wa vipindi vya Chaneli hiyo.
Amesema lengo la kuanzishwa kwa Chaneli hiyo ya Utalii ya Tanzania Safari ni kuitangazia dunia vivutio lukuki na vya aina ya pekee vilivyopo Tanzania ili watalii wa ndani na nje ya nchi wavutike kuvitembelea.