Maalim Seif kuapishwa kesho

0
206

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kesho Disemba 8 atamuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kumuapisha Maalim Seif itafanyika Ikulu Zanzibar.

Rais Mwinyi amemteua Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, uteuzi ulioanza Disemba 6 mwaka huu.

Uteuzi huo umezingatia  matakwa ya kifungu cha 9(3) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.