Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewateua Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Dkt. Mwinyi amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 66 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Uteuzi huo umeanza leo Disemba Saba.