Mahakama yatengua hukumu ya AY na Mwana FA

0
218

Mahakama Kuu imetengua hukumu iliyoamuru wanamuziki Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) na Ambwene Yesaya (AY), kulipwa Shilingi Bilioni 2.1 na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya kampuni hiyo kukiuka sheria za hakimiliki.

Jaji Joacquine De-Mello amekubaliana na rufaa ya kampuni ya Tigo kuwa mahakama ya wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Tayari kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Tigo iliishawalipa Mwana FA na AY fedha hizo.

Mwezi Aprili mwaka 2016, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Ilala, alitoa amri ya Wanamuziki hao kulipwa kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya kampuni ya Tigo.

Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo amesema atawaandikia barua Wanamuzìki hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa.