Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa-TAKUKURU wilayani
Kahama mkoani Shinyanga, imewaonya baadhi ya wastaafu
kuacha tabia ya kuchukua mikopo isiyokuwa na utaratibu unaoeleweka,
ili kukabiliana na baadhi ya Taasisi zinazotoa mikopo inayoumiza
wastaafu hao.
Mkuu wa TAKUKURU wilayani humo Cosmas Shauri amesema
hali hiyo imesababisha kuwepo kwa Taaisisi hizo kujipatia fedha isivyo
halali kutoka kwa watu wanaokopeshwa fedha hizo, jambo ambalo ni
kinyume na sheria na utaraibu wa nchi.