Vijana wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za ubunifu, ili kukidhi mahitaji ya maisha badala ya kutegemea ajira rasmi ambazo hazitoshi kwa kila mtu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa mara baada ya kutembelea kikundi Cha African Vema kinachojishughulisha na ushonaji wa mabegi katika wilaya ya Temeke.
Issa amesema lengo la kutembelea kikundi hicho, ni kusikiliza changamoto zao na kuona namna baraza linaweza kuwawezesha na kuwaunganisha na wadau mbalimbali wa uwezeshaji.