UEFA kuendelea leo usiku, Manchester United vs PSG, ni Kivumbi

0
227

Moja kati ya makundi magumu kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu huu ni kundi H. Hapa kuna Man United, PSG, RB Leipzig na Istanbul Basaksehir. United, PSG na Leipzig wote wananafasi ya kufuzu hatua ya 16 bora.

Mchezo wa kwanza kati ya PSG vs Man United uliochezwa nchini Ufaransa, United waliibuka kidedea kwa ushindi wa 2-1.

Msimu uliopita timu hizo zilikutana katika hatua ya 16 bora na United waliibuka na ushindi Old Trafford, lakini PSG wakaenda kupindua meza Stade de France na wakafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu barani Ulaya.

Licha ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya United, PSG walionesha uwezo katika mechi zilizofuata na wameshavuna alama 6 sawa na RB Leipzig wakati ambao United ni kinara wa kundi H akiwa na pointi 9 baada ya michezo 4.

Ushindi au matokeo ya sare katika mchezo huu, yataivusha United mpaka hatua ya 16 huku PSG wakihitaji ushindi ili kuweza kufufua matumaini ya kusonga mbele katika michuano hiyo ambayo msimu uliopita waliishia nafasi ya pili.