Tohara chanzo cha kupunguza maambukizi ya VVU

0
156

Katika kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI mkoani Simiyu, jumla ya wanaume laki moja na elfu tisini na nne (194,000) wamefanyiwa tohara kinga kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2019 huku taifiti zikionesha mwanaume aliyefanyiwa tohara, uwezekano wa kuzuia maambukizi ni asilimia sitini.

Hayo yamesemwa na kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, ambapo kimkoa yamefanyika katika uwanja wa halmashauri ya ji wa Bariadi.

Dkt. Kulemba akitoa taarifa ya hali maambukizi ya VVU mkoani Simiyu, amesema wilaya ya Maswa pekee yenye ushamiri mkubwa wa asilimia tatu nukta tatu (3.3%) na tayari wanaendelea kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za upimaji VVU ambapo hadi kufikia septemba 2020 ,jumla ya vituo 218 sawa asilmia 88 ,na tohara kwa wanaume ni moja ya mkakati wa kupunguza maambukizi mapya