Jela miaka 2 kwa kumkata viwembe mtoto wa kambo

0
336

Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemtia hatiani Agnes Damian (40) mkazi wa Mji Mwema Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kosa la kumkata kwa wembe sehemu mbalimbali za mwili binti wa miaka 15 ambaye ni mtoto wa mume wake.

Katika hukumu hiyo iliyodumu kwa takribani dakika 18 ikisomwa na Hakimu Eva Mushi amesema adhabu hiyo inapaswa kuwa fundisho na onyo kwa wanatenda matukio ya kikatili hasa kwa watoto.

Hakimu Mushi ameongeza kuwa hukumu ya kesi namba 95/2020 imezingatia sheria ya adhabu kifungu 225 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisbo mwaka 2019.

Tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka usiku ambapo mtuhumiwa aliingia chumbani na kufanya ukatili huo akimtuhumu kuwa binti huyo alimpiga mwanae na kwamba lazima ampe onyo.

Imebainishwa kuwa binti huyo alijeruhiwa kwa wembe maeneo ya miguu, mapaja na mgongoni

Kesi hiyo ilikuwa chini ya mawakili wa serikali Happiness Mayunga na Crement Masua ambapo mara baada ya hukimu wakili Masua ameeleza kutoridhishwa na kifungo cha miaka miwili huku akioneshwa kuridhishwa na faini ya milioni 5.

Kabla ya adhabu hiyo, Agnes aliomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa anatunza watoto wawili, ni yatima na hivi karibu amepona ugonjwa wa kupoza japo hajawa timamu asilimia mia moja.

Kwa kuzingatia ushahidi wa watu sita wakiwemo baba mzazi, majirani, daktari na askari, hakimu alimuhumuku kifungo cha miaka 2 jela na faini milini 5 na kwamba iwe fundisho kwa wengine.