Modric kumaliza soka lake Madrid

0
255

Kiungo wa Real Madrid raia wa Croatia, Luka Modric, ameendelea kusema anataka kuona anamalizia kipindi chake cha kucheza soka kwenye kikosi hicho ikiwaimebaki miezi nane na kikosi hicho.

Hata hivyo, bado imekuwa ikisemwa kuwa kuna uwezekano wa kiungo huyo kujiunga na Tottenham Hotspur mwishoni mwa msimu huu.

Mshindi huyo wa Ballon d’Or 2018, inaelezwa kuwa, bado ana muda wa kucheza zaidi kwa msimu mmoja kabla hajatundika daruga ambapo hivi sasa ana miaka 35.

“Bado najisikia vizuri sana, suala la michezo ambayo sijacheza nafikiri haya ni maamuzi ya kocha na
siyo mimi, kama ikitokea natakiwa kucheza nitaitumikia timu yangu kwa moyo wote.

“Nimekuwa nikisema mara nyingi na narudia kusema kuwa ninataka kuona namaliza kipindi changu cha soka hapa,” amesema Modric.