Bilioni 41 zimewekwa na serikali ili kufanya marekebisho ya Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Iringa utakaobadilisha taswira ya mkoa huo na kuongeza uchumi wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
“Tumekusudia kukuza utalii Nyanda za Juu Kusini na mkoa wa Iringa utakuwa sehemu muhimu ya kupokelea watalii, hivyo lazima kuwa na uwanja mzuri na wenye viwango bora,” ameeleza Kasesela
Kwa upande wake mkandarasi wa ujenzi wa uwanja huo, Zhang Cheng amesema mradi huo unatarajia kukamilika Machi 2022.
Sambamba na ajenda ya zoezi la karibu kusini, mkoa wa Iringa tayari umeanza kujipambanua katika uwekaji mazingira rafiki kwenye vivutio mbalimbali vya utalii.