Rais Magufuli afanya uteuzi wa wabunge wawili

0
262

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa wabunge wawili kwenye Bunge la Tanzania.

Kwanza Rais Magufuli amemteua Humphrey Polepole kuwa Mbunge Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Polepole ni Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM – NEC, itikadi na uenezi.

Taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa Rais Magufuli pia amemteau Riziki Lulida kuwa Mbunge Katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bi Lulida alikua pia mbunge wa viti maalumu Katika Bunge la 11.

Wateuliwa wote wataapishwa kwa amujibu wa sheria na taratibu za Bunge.