Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watano akiwemo Rahel Matalaka mkazi wa kijiji cha Ikelege wilayani Misungwi kwa tuhuma za kumpiga hadi kusababisha kifo cha mtoto wake Maliatabu Constantine, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Ikelege.
Kamanda wa polisi wa mkoa Mwanza, – Jonathan Shanna amesema kuwa Rahel anatuhumiwa kumpiga Maliatabu sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo, baada ya kufikishiwa malalamiko kuwa ameiba maembe kwa jirani.
Kamanda Shanna ameongeza kuwa baada ya kusababisha kifo cha mtoto wake, Rahel alimtundika mtoto wake juu ya mwembe kwa kutumia kipande cha kanga ili kupoteza ushahidi.