Watumishi TBC waitangaza njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro

0
296

Baadhi ya watumishi wa TBC wamepanda Mlima Kilimanjaro (Hadi kituo cha Mandara) kupitia Njia ya Marangu kwa lengo la kuitangaza njia hiyo ambayo imeshinda tuzo huko nchini China ikiwa njia bora zaidi kupanda kwenye mlima huo.

Kuna njia tano za kupanda Mlima Kilimanjaro ambazo ni Marangu, Machame, Umbwe, Rongai na Lemosho. Kati ya hizo, njia ya Marangu ndiyo kongwe zaidi.

Unapopanda mlima kupitia njia ya Marangu uwapo getini utaweza kuona picha za kumbukumbu mbalimbali ikiwemo watu wa kwanza kupanda mlima na vivutio vingine kama maporomoko ya maji kabla hujaanza safari ya kufika kileleni.

Mlima Kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi Afrika na mlima mrefu zaidi duniani uliosimama wenyewe ukiwa na urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.