Kijana wa miaka 17 nchini India anashikiliwa na polisi kwa kosa la kujaribu kumuua mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 16.
Kamanda wa polisi, Prakash Surya ameieleza NDTV kuwa ndugu hao wawili waligombana baada ya kaka mtu kumkataza mdogo wake kuwasiliana na Amir, ambaye ni shemeji wa dada yao mkubwa. Katikati ya malumbano hayo kijana huyo alichukua bastola na kumfyatulia dadake.
Binti huyo anasema kuwa yeye alikuwa akiwasiliana na Amir mara kwa mara kwa kutumia simu ya baba yake, jambo ambalo kaka yake hakuwa akiliafiki.
Majeruhi amelazwa katika hospitali ya Jag Pravesh Chand nchini India