Jela Miaka 20 kwa kusafirisha raia wa kigeni

0
192

Wakazi wawili wa wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya shilingi milion 20 kila moja kwa kosa la kusafirisha raia wa kigeni walioingia nchini bila kibali.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Tanga Emilius Mchauru.

Wananchi hao ni Rashidi Bakari(20) na Ally Omary(21).

Aidha mwananchi mwingine aliehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi milion mbili, ni Haruna Zuberi (40)mkazi wa Muheza yeye alihusika kuwapa hifadhi raia hao.

Kwa upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Tanga Mbaraka Batenga, yeye amesema katika kipindi cha miezi sita jumla ya raia wa kigeni 227 walikamatwa mkoani Tanga wakitokea nchi za Kenya,Rwanda,Pakstani na Ethiopia.