IGP Sirro akutana na IGP wa Msumbiji

0
235

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amekutana na mgeni wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Msumbiji, IGP Bernardino Rafael katika kikao kazi cha ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili kilichofanyika mkoani Mtwara.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kitajikita zaidi kujadili hali ya usalama ya mpaka wa Tanzania na Msumbiji ambapo kwa siku za hivi karibuni kulitokea vurugu.