Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefaanya uteuzi wa baraza la mawaziri ambapo baraza hilo lina jumla ya wizara 15.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar, Dkt. Shein amesema kuwa amefanya mabadiliko mbalimbali ikiwa ni kupangua baadhi ya wizara, kuhamisha nyingine, lengo likiwa kuongeza ufanisi katika kuwatumikia Wazanzibari.
Walioteuliwa kuongoza wizara mbalimbali ni,
- Ofisi ya Rais Uchumi na Uwekezaji – Mudrik Ramadhan Soraga
- Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Talawa za Mikoa na Vikosi vya SMZ- Masoud Ali Mohammed
- Ofisi ya Rais Katiba, Sheria na Utumishi na Utawala Bora- Haroun Ali Suleiman
- Ofisi ya Rais Fedha na Mipango – Jamal Kassim Ali
- Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Dkt. Khalid Salum Mohammed
- Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo- Dkt. Soud Nahoda Hassan
- Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali- Simai Mohammed Said
- Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni na Michezo- Tabia Mwita Maulid
- Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi- Riziki Pembe Juma
- Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale- Leyla Mohammed Mussa
- Wizara Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi-Rahma Kassim Ali
- Wizara Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Abdallah Hussein Kombo
- Wizara ya Maji na Nishati- Suleiman Masoud Makame
- Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda- (Ipo wazi)
- Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Watoto- (Ipo wazi)
Dkt. Mwinyi amesema kuwa nafasi mbili kwenye wizara alizoziacha wazi ni kwa ajili ya Chama cha ACT-Wazalendo, na kwamba endapo walioshinda nafasi za Uwakilishi watasajiliwa katika Baraza la Wawakilishi ndani ya muda wa kikatiba, atawateua kuunda serikali.
Kuhusu kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais kutoka chama cha upinzani kitakachopata zaidi ya asilimia 10, Dkt. Mwinyi amesema kuwa wamekiandikia barua chama cha ACT-Wazalendo wawasilishe jina la mtu atakayeshika nafasi hiyo kama katiba inavyotaka, lakini chama hicho hakijatoa jina.
Hafla hiyo imefanyika Ikulu, Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.