Picha: Emmanuella ampa mama yake zawadi ya jumba la kifahari

0
3662
Mchekeshaji kutoka Nigeria, Emmanuella Samuel

Mchekeshaji maarufu Nigeria na Afrika, Emmanuella Samuel ambaye sasa ana umri wa miaka 10 amemjengea mama yake nyumba ya kifahari na kumpa kama zawadi ya mapema ya Sikukuu ya Krismasi.

Emmanuella amenukuliwa akisema amejenga nyumba hiyo kupitia faida ya kazi yake ya sanaa ya kuchekesha.

Mama wa mchekeshaji huyo amekuwa akionesha ushirikiano katika kukuza kipaji cha binti yake tangu alipoanza kuchekesha akiwa na miaka mitano.