Dkt. Hussein Mwinyi awasili Dodoma kuhudhuria uzinduzi wa Bunge

0
220

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasili Jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Dkt. Hussein amepokewa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli anatarajiwa kulizindua Bunge hilo la 12 kesho Novemba 13.

Katika safari hiyo, Dkt. Hussein Mwinyi amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi.