Vunja Bei agawa vyombo kwa watumishi wa Muhimbili

0
448

Shija Kamanija maarufu Vunja bei atoa zawadi ya vyombo kwa wafanyakazi wote wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Vunja Bei amesema ni zoezi hilo ni muendelezo wa ahadi yake ya kuunga mkono juhudi za Rais Job Magufuli katika kuwahudumia Watanzania.

Amesema ameona ni vyema kuwakumbuka watumishi wa sekta ya afya na kuwazawadia vyombo vya ofisini na binafsi kwa wafanyakazi wote wa taasisi hiyo.

“Hawa madaktari na wauguzi wamefanya kazi nzuri sana mwaka huu. Hivi karibuni nchi yetu ilikumbwa na ugonjwa wa Corona lakini hawa watu walifanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya Watanzania,” amesema Vunja Bei.

Vuja Bei ameamua kutoa zawadi za vyombo kwenye taasisi za kiserikali hasa upande wa sekta ya afya, elimu na ulinzi na usalama.

Novemba 9 mwaka huu aligawa vyombo kwa walimu na wanafunzi wa baadhi ya shule za serikali jijini Dar es Salaam.