Vunja Bei aunga juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano

0
263

Ikiwa ni lengo la serikali ya awamu ya tano kuwa na uwepo wa mazingira mazuri kwa walimu na wanfunzi shuleni, Shija Kamanija maarufu kwa jina la Vunja Bei ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja Bei, wauzaji wa vyombo bora Tanzania wamegawa bidhaa hizo kwa walimu na wanafunzi jijijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunja Bei Shija Kamanija akimpa zawadi ya vyombo Mwalimu

Kampuni hiyo imesema kuwa imefanya hilo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli katika kutoa elimu bure kwa watoto wanaosoma shule za Serikali.

Walimu na wanafunzi waliopewa zawadi hizo wameishukuru Vunja Bei na kuahidi kuendelea kutumia bidhaa zao.