Watu zaidi ya 50 wanusurika kifo katika ajali basi la Abood

0
1059

Watu zaidi ya 50 wamenusurika kifo baada ya basi la Abood (T 266 DBV) walilokuwa wakisafiria kutoka Morogoro kwenda Dar es salaam kupinduka mara mbili katika eneo la Ruvu wilayani Kibaha.

Baadhi ya abiria walionusurika katika ajali hiyo wameiambia TBC kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi wakati dereva wa basi hilo akipita lori lililokuwa mbele yake bila tahadhari na kukutana na gari lingine na alipojaribu kulikwepa basi hilo likayumba na kumzidi nguvu na kupinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema idadi kamili ya watu waliojeruhiwa zaidi ni wawili.

Kamanda Wankyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliosababishwa na dareva basi hilo ambaye alikuwa akikimbizana na mabasi mengine mawili ya kampuni hiyo yote yakitokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam.

Kufutia ajali hiyo kamanda hiyo ameligiza jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuwatafuta na kuwakamata mara moja madereva wa mabasi hayo.