Bunge la 12 kuanza rasmi Novemba 10, 2020

0
536

Rais Dkt. John Magufuli anatarajiwa kufungua Bunge la 12 baada ya wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua wabunge watakaowawakilisha kwa kipindi cha miaka mitano.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge imeeleza kuwa siku hiyo shughuli mbalimbali zitafanyika ambazo ni pamoja na kusomwa kwa tangazo la Rais la kuitisha Bunge, uchaguzi wa spika na naibu spika, kuthibitishwa kwa uteuzi wa waziri mkuu.

Shughuli nyingine ni kiapo cha uaminifu kwa wabunge wote.

Wabunge wateule wametakiwa kwenda na nyaraka mbalimbali ikiwemo hati ya kuchaguliwa/kuteuliwa kuwa mbunge, nakala ya kitambulisho cha Taifa na vyeti vya elimu.