Trump adai kura zake zimeibwa

0
256

Leo ni siku ya tatu tangu kuanza kwa zoezi la kuhesabu kura nchini Marekani baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika Novemba 3 mwaka huu ambapo mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden anaongoza katika katika kura maalum maarufu kama ‘electoral vote.’

Rais Donald Trump ambaye anagombea kwa muhula wa pili amekilaumu chama Democratic kuwa kinamwimbia kura na kwamba hatokubaliana na matokea ya kushindwa.

Trump ametoa tuhuma hizo bila kuwa na ushahidi wowote, na madai yake yamejikita katika uhalali wa idadi kubwa za kura za awali zilizopigwa kwa njia ya posta ambazo ni zaidi ya zile ambazo zilihusisha watu kwenda kupiga moja kwa moja katika siku ile ya uchaguzi ya Novemba 3.

Katika madai yake, Trump amesema atachukua hatua za kisheria ili kusitishwa zoezi la kuhesabu kura kwa  kukosa imani na matumaini dhidi ya wafuasi wa Joe Biden ambao wameanza kusherehekea nje ya kituo kikuu cha kuhesabu kura.

Kwa upande wa ke Biden amewataka raia wa Marekani kutulia na kuacha zoezi la kuhesabu kura.