Shambulio la kigaidi latikisa Austria

0
260

Watu wawili wamefariki na wengine 14 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia maeneo sita tofauti mjini Vienna, Austria.


Kansela Sebastian Kurzwa wa Austria ametaja shambulio hilo kuwa la kigaidi, maafisa polisi ni kati ya watu waliojeruhiwa katika shambulio hilo.


Mashuhuda wa shambulio hilo wanasema washambuliaji walifyatua risasi katikati ya umati wa watu waliokusanyika katika baa na kusababashisha taharuki ya watu kukimbia huku na huku ambapo wengine wamejeruhiwa vibaya.


Shambulizi hilo limetokea saa chache tu kabla ya Austria, kutangaza masharti mapya ya kupambana na janga la Corona, kutokana na ongezeko la virusi hivyo nchini humo.


Serikali imetoa wito kwa wakaazi kukaa nyumbani na kukwepa usafiri wa umma  katikati mwa jiji la Vienna.


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Austria Karl Nehammer amezungumza na waandishi wa habari na kusema imekuwa siku ngumu sana nchini humo